Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Bw. Profesa John Nkoma
akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Inocent Mungi Meneja
Mawasiliano wa TCRA.
………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Ongezeko la matumizi
ya Intaneti kwa watanzania nchini limeongezeka kutoka watumiaji laki
tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 Kwa takwimu za
hivi karibuni.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Profesa John
Nkoma wakati wa Kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mawasiliano
yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Profesa
Nkoma amesema kuwa wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni
katika kujifunza, kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandaoi ya
kijamii ikiwemo Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na Blog mbalimbali
zitoazo habari mbalimbali za kimaendeleo, burudani na michezo.
“Matumizi
haya ya intaneti yamenufaisha watanzania walio wengi kwani ni fursa
murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari
mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleat
amani miongoni mwa watanzania”. Profesa Nkoma alisema.
Profesa
Nkoma aliwaasa baadhi ya watu wachache wenye tabia ya kutumia
mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, radio, runinga na mawasiliano
mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchochea vurugu , kuchonganisha
watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo ya ukweli,
kupotosha jamii na maendeleo kwa ujumla.
Aidha,
Profesa Nkoma amewatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano
vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya kielectroniki
(EPOCA) ya mwaka 201 ni makosa.
“Kampeni
hii, Mamlaka inakusudia kuwasihgi wananchi kuhakikisha wanatumia
mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni
mwa watanzania”. Profesa Nkoma alisisitiza.
Kwa
upande mwingine Profesa. Nkoma alizindua wimbo wa video wenye ujumbe wa
“Futa na delete meseji kabisa”, wimbo ambao umeandaliwa na wasanii
Mrisho Mpoto na Banana Zorro wenye lengo la kuwataka wananchi kutumia
mitandao ya kijamii vizuri kwa kuepuka uchochezi na matusi katika
kuitumia.
Profesa
Nkoma amewasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa
wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki unaopelekea kuvuruga amani,
watoe taarifa kwa vyombo husika, kisha wafute ujumbe huo ili usienezwe
kwa wengine kwani uatkuwa sehemu ya uhalifu.
Siku
za hiuvi karibuni ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa
kasi sana na katika kipindi kifupibzimekuwa sana na kuwafikia
watanzania wengi zaidi kutoka laini za simu za mkononi milini tatu tu
mwaka 2000 hadi kufikia laini milioni 28.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)