Kama kawaida: Philip Lahm (katikati) akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la mapema
Mwendo mzuri: Kikosi cha Pep Guardiola kimeonekana kuwa imara zaidi na kuwatwanga Barcelona
Hovyo kweli: Nahodha wa Barca, Lionel Messi alicheza vibaya katika kipindi cha kwanza na kutolewa
Chuma cha pili: Mario Mandzukic akifunga bao la kuwazamisha wanaume wa Katalunya
Ufunguzi wa mabao: Lahm akishangilia baada ya kuifungia klabu yake na kuongoza kwa 1-0
Kazi na dawa: Thiago (kushoto)na Boateng (kulia) wakimghasi MessiVita ya kuwania gozi: Frank Ribery wa Bayern akiwania mpira na Marc Bartra wa Barca.
Imara kama kawaida: Guardiola anaonekana kuwa na kazi nyepesi na Bayern yake, wametumia kikosi cha moto kuwashinda Barca
Burudani kama kawaida: Wanamuziki wa asili wakivalia kitamaduni wakitumbuiza kabla ya mchezo kuanza
Kivutio cha wengi: Messi alianza katika kikosi cha kwanza cha Barcelona, Allianz Arena.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
wa wekundu wa kusini mwa Ujerumani, “Bavarians” Bayern Munich, Joseph
Pep Guardiola ameifunga klabu yake ya zamani ya FC Barcelona mabao 2-0
katika mechi ya kirafiki uwanja wa Allianz Arena jijini Munich nchini
Ujerumani .
Nahodha
Philipp Lahm alifungua bao la kwanza dakika ya 14, lakini hadi dakika
45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Bayern walikuwa mbele kwa bao
moja. Bao
la pili lilifungwa na Mario Mandzukic katika dakika ya 87 na kipute
hicho kumalizika kwa ushindi kwa Bayern ambao wanaonekana kuwa na morali
kubwa ya kufanya makubwa msimu wa 2013/2014.
Japokuwa
Bayern wamepata wamesubiri mpaka dakika za lala salama kutia kambani
bao la pili, lakini walifanya kazi nzuri ndani ya dakika zote 90 na hii
inadhihirisga kwamba msimu ujao utakuwa mzuri kwao, hivyo wapinzani wao
wa barani Ulaya wanatakiwa kuchukua tahadhari kubwa.
Kikosi
cha Bayern Munich: Neuer (Starke 46), Rafinha, Dante (Van Buyten 59),
Boateng, Alaba, Thiago, Lahm (Gustavo 59), Kroos, Ribery, Robben
(Shaqiri 46), Muller (Mandzukic 46).
Mabaol: Lahm 14, Mandzukic 87. Kikosi
cha Barcelona: Pinto (Oier 46), Montoya (Kiko 46), Bartra (Gomez 46),
Mascherano (Planas 46), Adriano (Patric 46), Song (Espinosa 46), Sergi
Roberto (Ilie 46), Dos Santos (Quintilla 46), Tello (Joan Roman 46),
Messi (Dongou 46), Alexis (Dani Nieto 46
Bayern
walitawala sana mchezo huo na huenda wangepata mabao mengi zaidi kama
safu yao ya ushambuliaji ingetulia kubadili nafasi walizopata kuwa
mabao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)