MUDY MATUMLA |
BONDIA
Mohamed Matumla pichani anatarajia kupanda ulingoni julay 6 mwaka huu
katika ukumbi wa DDC Keko kwa ajili ya kupambana na Hamis Mohamed kutoka
GYM YA MZAZI mpambano huo wa raundi nane utakuwa mkali sana kutokana
na kuwa mabondia wote wana uzoefu wa kutosha Matumla anaetokea katika
familia yenye vipaji lukuki vya masumbwi Hamisi anatokea katika GYM
iliyojihakikishia wanachukua mikanda yote nchini na nje ya nchi
Akizungumza na mwandishi wetu mwandaaji
wa mpambano huo Shabani Adios 'Mwaya mwaya' amesema mpambano huo
utasindikizwa na mabondia mbalimbali wanaotamba katika masumbwi
Mabondia hawo ni Shafii Ramadhani atakayemenyana na Juma Fundi huku Swaleh Mkalekwa akipambana na Cosmas Kibuga
mpambano huo unaotarajiwa kuwa wa kukata
na shoka wa raundi sita umekuwa wa kusisimua na kuzagaa katika vinywa
vya mashabiki wa mchezo huo Huku bondia Mohamed Matumla
akimtahadhalisha mpinzani wake kuwa siku hiyo ato kuwa na msalia mtume
kwani kawaida yake inajulikana Matumla mpaka sasa amepambana mapambano
13 akidroo matatu na kushinda 10 ata hivyo ame sisitiza kumuhangamiza
mpinzani wake mapema kadri iwezekanavyo na kuwaomba wapenzi wa mchezo
huo waje mapema kushudia anavyo mmaliza vinginevyo watakosa uhondo wa
masumbwi Mbali na kuwepo na mpambano huo Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' atasambaza DVD za mafunzo ya
mchezo wa masumbwi
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa
ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na
mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana
DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika
masumbwi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika
makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la
Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani
kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha
kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza
zaidi mchezo huo
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo ya mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super
D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)