Edwin Mosha
Wakati mwingine ndugu zangu wadau hakuna ambaye hafurahii
kukua kwa teknolijia hasa ya upashanaji habari kwa njia mbalimbali ambazo
zitamsaidia mtu kufahamu matukio mbalimbali ambayo kimsingi yatamtoa hapo alipo
na kuhabarika zaidi
Lakini hali hii ya kukua kwa kasi imekumbwa na maudhi ambayo
nina uhakika si mimi peke yangu nimeyaona ila wapo waliotangulia na wakasema,
lakini pia imefika zamu yangu kusema na nina imani kuwa hata wenzangu
wanakumbana nayo ipo siku nao watasema
Ongezeko la mitandao tando (blogs) hakuna asiyejua kuwa ni
msaada mkubwa wa kuwafikishia watu habari kama utatimiza malengo yako kwa kuwa
ulipokuwa na mpango wa kufungua hiyo blog yako lazima ulikuwa na malengo ambayo
bila shaka ulikaa chini na kuona kuwa utayamudu
Nichukulie mfano kwa nchi yetu ambayo ni kubwa, si kila
habari unaweza kuipata kwa kufika eneo la tukio na ukaichukua kutoka kwenye
vyanzo husika, labda uwe na waandishi wa habari katika mikoa ama wilaya zote za
Tanzania, lakini kwa kuwa wamiliki wengi wa mitandao tando(blogs) hawana uwezo
huo, inawalazimu kuchukua habari ambazo tayari zimewekwa kwenye mitandao ya
mwanalibeneke mwenzako na kuziingiza kwenye blogs zao, kwa maana nyingine
tunategemeana
Hili si tatizo bali nachoona mimi kuwa ni tatizo ni kuwa
baadhi ya wanalibeneke(bloggers) wengi wanakosea hata “kucopy” na “kupaste”
jambo ambalo limekuwa likiboa wasomaji wa blog zetu kwa kuwa unaweza kukuta
habari moja imekosewa kwenye zaidi ya blog 50 ambazo zimeweka habari hiyo hiyo,
jambo linaloshiria kuwa mtu ana copy habari na kuipaste kwake bila hata yeye
mwenyewe kuisoma, sasa kama wewe huisomi na kuihariri je unataka nani aisome na
kuirekebisha?
Na si hilo tu, pia si kila habari iliyopo kwenye blog ya
mwenzako inatakiwa iwepo kwenye blog yako kwa kuwa kama ndiyo hivyo je ni kwa
nini kusiwe na blog moja itakayokuwa na habari zote, kwa kuwa unakuta habari
zilizoko kwenye blog moja ndiyo hizo hizo zipo katika blog zaidi ya 20 sasa unajiuliza
tofauti za blog zetu kwa sasa ni majina ama ni nini? Ninaposema si kila habari
lazima iwe kwenye blog yako namaanisha zipo habari ambazo mmiliki wa mtandao
kazitafuta angalau kutofautisha blog yake na nyingine, mfano kakuta mifugo
inazurura mitaani akaipiga picha na kuziweka kwenye blog yake, unakuta
wamezinakili na kuziweka kwao, tena wakati mwingine bila hatimiliki ya mwenye
picha ama ulipoinakili, sasa unajuuliza hivi wamiliki hawa hawajui kutofautisha
habari za “kucopy” na za kuacha?
Huu si muda wa kuwaudhi wasomaji kwa kukuona kuwa huna
ubunifu na namna ya kuelewa ni jinsi gani ya kunakili habari na habari ipi uiache,
mfano rais akiwa na ziara sehemu fulani mathalani hapa nchini, lile ni tukio
ambalo linatazamwa na nchi nzima kufahamu kinachoendelea na wanahabari
wanaokuwa naye ndiyo tunaowategemea kwa habari za ziara hiyo, ambapo hata
ukizinakili zinaleta mantiki, lakini usisahau kutoa hati miliki ya mwenye
habari
Hebu tubadilike na tuone huu ni muda wa kutumia vizuri
libeneke zetu ili zizidi kuwavutia watu, na kama unaona huwezi, hebu jifunze
kwa wanaoweza wakuelekeze halafu uje kuendelea na kitu chenye ubora na mvuto
kwa wasomaji
Ni hayo tu wadau
Edwin Moshi
EDDY BLOG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)