MKURUGENZI WA SOKO LA AJIRA, MIPANGO NA MAENDELEO WA VETA ENOCK KIBENDELA ATEMBELEA BANDA LA VETA KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOONYESHWA KATIKA MAONESHO YA SABASABA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKURUGENZI WA SOKO LA AJIRA, MIPANGO NA MAENDELEO WA VETA ENOCK KIBENDELA ATEMBELEA BANDA LA VETA KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOONYESHWA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

01Umeonaa! Hivi ni kazi yangu nikimaliza najiajiri. Ndivyo anavyoelekea kusema mwanafunzi Paulina Emmanuel anayejifunza masuala ya ubunifu wa mavazi na mitindo katika chuo cha VETA Chang’ombe Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na maendeleo wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bw. Enock Kibendela alipotembelea banda a VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es Salaam02Mwanafunzi Ernest Maranya wa VETA Chang’ombe akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya Sabasaba Dar es Salaam  akionyesha kifaa cha elimu ya mfumo wa jua na sayansi ya anga jinsi kinavyofanya kazi. 03Mkufunzi wa masuala ya hoteli na Utalii katika chuo cha VETA Njiro, mkoani Arusha Theonestina Raphael akitoa maelezo kwa askari polisi waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es Salaam. 04Tukiongeza ufundi kidogo tutakuwa tumemaliza kazi! Ndivyo anavyoonekana kusema Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na maendeleo wa VETA, Bw. Enock Kibendela mwenye kofia alipokuwa akikagua bidhaa za Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya sabasaba, Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mrtibu wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam Florence Kapinga na Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho Abdul Mollel na Afisa Uhusiano wa VETA Dorah Tesha 05Mafunzo kwa watu wenye mahitaji maalum yanatolewa hivi! Mwalimu Kintu Kilanga mwenye kofia akimueleza Mkurugenzi wa Soka la ajira, mipango na maendeleo wa VETA Bw. Enock Kibendela kuhusu mbinu wanazotumia kumfundisha mwanafunzi Range Jackson (kushoto) mwenye tatizoo la Hyperactive. Hyperactive ni tatizo ambalo linasababisha mtoto kuwa na uelewa dhaifu wa masuala mbalimbali.   06Moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Range Jackson mwanafunzi wa VETA  Chang’ombe anayesoma mafunzo maalum ya uchomeaji. 09Hakuna tena kupeleka mchanga wa dhahabu nje: Mchimbaji mdogo kutoka Nyarugusu mkoani Geita Michael Nsangano akionyesha mashine ya kuchakata dhahabu ambayo ni maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Mashine hiyo ni moja ya teknolojia inayoonyeshwa na VETA kwenye banda lake lililopo Sabasaba, Dar es Salaam. 010Hakuna tena kupeleka mchanga wa dhahabu nje: Mchimbaji mdogo kutoka Nyarugusu mkoani Geita Michael Nsangano akionyesha mashine ya kuchakata dhahabu ambayo ni maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Mashine hiyo ni moja ya teknolojia inayoonyeshwa na VETA kwenye banda lake lililopo Sabasaba, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages