Usiku
wa leo dunia itapata nafasi ya kushuhudia mechi ya kukata na shoka
kati ya timu za mtaifa mawili zenye utajiri wa vipaji na historia nzuri
katika soka la kimataifa. Spain vs Brazil ni mechi ambayo ilikuwa
ikisubiriwa sana na wapenda soka hasa wa kizazi cha sasa.
Brazil
ilitawala sana miaka mingi iliyopita wakiwa mabingwa wa mara tano wa
kombe la dunia, lakini sasa Spain La Roja ndio timu inayotawala kwenye
soka la kimataifa - wakiwa hawajafungwa kwenye mechi yoyote ya
kimashindano tangu mwaka 2010 - wakichukua makombe makubwa matatu (Euro
2008, World Cup 2010, Euro 2012) katika kipindi cha miaka ipatayo
mitano, na kesho wapo katika harakati za kuandika historia ya kutwaa
makombe yote manne makubwa watakapocheza fainali ya kombe la mabara
dhidi ya Brazil kwenye uwanja wa Maracana - Rio de Jeneiro. Je Brazil
watarudisha utawala waliopoteza au Spain wataendelea kushikilia usukani
mwa soka la kimataifa?.
Katika
michezo nane ambayo timu hizi zimekutana, spain wameshinda mara moja tu
- zamani sana mwaka 1934. Lakini kipindi hicho Spain lilikuwa taifa
dogo sana kwenye soka - Brazil na Uholanzi wakiwa wapo juu. Mechi yao ya
mwisho iliyozikutanisha timu hizi mbili ilikuwa mwaka 1999, iliisha kwa
sare 0-0. Brazil kwa sasa hawapewi nafasi kubwa ya kuifunga Spain -
ingawa usiwadharau Selecao ambao hawajafungwa kwenye ardhi yao katika
mechi nne za kimashindano dhidi ya Spain - wakishinda mechi 3 na kutoa
sare 1.
JE WAJUA?
-
Brazil wameshinda 11 mfululizo za kombe la mabara. Pia wameshinda
michuano micwili iliyopita ya mashindano haya (2005 and 2009), na hii ni
fainali yao ya 3 mfululizo.
-
Spain wamecheza mechi 29 za mashindano bila kufungwa - hawajapoteza
mechi tangu walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza ya kombe la
dunia 2010.
-
Spain ndio timu inayoongoza kupiga pasi zilizokamilika katika michuano
hii - asilimia 92. Wamepiga pasi 3052 ukilinganisha na Brazil waliopiga
pasi 1783. Watani wa 84.5%.
- Spain wameruhusu mashuti nane tu yaliyolenga lango lao katika michezo minne waliyocheza kwenye michuano hii mpaka sasa.
-
Torres amefunga mabao nane katika historia ya kombe la mabara. Ni
Cuauhtémoc Blanco (Mexico) na Ronaldinho (Brazil) ambao wamemzidi kwa
kufunga mabao (9).
-
Fred amefunga mara nane katika michezo 10 aliyoichezea Brazil. Matatu
kati hayo 10 ameyafunga kwenye michezo miwili iliyopita kwenye kombe la
mabara. Habari/Picha Kwa Hisani ya Shaffih Daud Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)