Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema wakiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu
(Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Freeman Mbowe na Godbless Lema wakiwa katika Uwanja wa Soweto jana
mchana wakati zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali likiendelea chini ya
usimamizi wa wataalamu toka jeshini.
Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako
kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo
zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo
tanki hilo lilishambuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii
ya matangazo lina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu
chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bwana Benny akiwa hospitali.
James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani.Picha zote na Arusha255 Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)