Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani Askari 29 wa Magereza kanda ya Nyanda za Juu Kusini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani Askari 29 wa Magereza kanda ya Nyanda za Juu Kusini

Msafara wa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja ukiwasili katika viwanja vya Chuo cha ufundi Ruanda Jijini Mbeya kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari wa Jeshi la Magereza 
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  Akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na maaskari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari.

 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  akipokea Salam za heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya
 Baadhi ya Maaskari wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  (ambaye haonekani pichani) wakati wa hafla ya kuwatunuku nishani.
 Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira Rungwe wakitumbuiza katika Sherehe hizo 


 Baadhi ya Maaskari wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na maofisa wakifuatilia kwa umakini Sherehe za    kutunuku nishani 
 Baadhi ya Maaskari wakisubiri kutunukiwa nishani kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja 
SACP C. A Keenja akitaja majina 29 ya Maaskari wanaotakiwa kutunukiwa Nishani ya Utumishi uliotukukuka Tanzania, Utumishi Muda Mrefu Tanzania, Utumishi mrefu na tabia njema na Mwenge wa Uhuru daraja la nne.

 Askari Mwanamke akitembea kwa ukakamavu kuelekea eneo linalotumika kutunukia Nishani kwa Maaskari wa Jeshi la Magereza 
 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (kulia) akimvisha nishani ya utumishi ulio Tukuka Tanzania ACP Hawa M. Simon ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.

 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akimvisha Nishani ya utumishi mrefu na tabia njema SGT Yusufu F. Nzunda kutoka chuo cha Magereza Kiwira 

 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimpongeza Askari mara baada ya kutunukiwa nishani ya utumishi mrefu na Tabia njema.
 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akiwa katika picha ya pamoja na Maaskari 29 waliotunukiwa Nishani mbalimbali 
  Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wastaafu.

Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliotunukiwa Nishani

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages