Baadhi ya makatibu wakuu wa mikoa wa vyama vya soka vya mikoa inayoshiriki michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars wakifuatilia kwa makini kanuni za mashindano hayo wakati wa semina elekezi iliyofanyika TFF leo.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando akiongea na makatibu wakuu wa mikoa na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TFF leo.
Katibu mkuu mkoa wa kisoka wa Temeke Mbarouk Mhamed (kulia) akichukua karatasi wakati wa kupanga makundi na ratiba ya michuano ya Taifa ya Airtel Rising Stars iliyopangwa kuanza mwezi Julai, 2013 uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Kushoto ni katibu wa DRFA Msafiri Kondo.
FAINALI
za Taifa za michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 za Airtel
Rising Stars zimepangwa kuanza kutimua vumbi uwanja wa Kumbu Kumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam Julai 2 kwa mabingwa watetezi Temeke
wavulana kupambana na Kinondoni.
Akizungumza
wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars 2013 iliyofanyika Juni
mosi katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF), Ofisa Maendeleo wa shirikisho hilo Bw. Salum Madadi alisema ARS
ngazi ya mikoa imepangwa kuanza Juni 15 hadi 29.
Mikoa
inayoshiriki Airtel Rising Stars mwaka huu kwa upande wa wavulana ni
mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Mikoa mingine ni Morogoro
Mwanza na Mbeya ambapo kila mkoa unatakiwa kushirikisha timu sita. Usajili wa timu umepangwa kuanza rasmi kesho Juni 2 na kumalizika Juni 11.
Kwa upande wa timu za wasichana, alisema, mikoa itakayoshiriki ni Tanga, Kigoma na Ruvuma na mikoa yote inayoshiriki Airtel Rising Stars mwaka huu iliwakilishwa kwenye semina elekezi na makatibu wakuu ambao walipata fursa ya kupitia kanuni na taratibu za michuano hiyo ya vijana.
Upangaji
wa ratiba uliofanyika leo ni wa fainali za taifa pekee kwa kuwa
mashindano ya ngazi ya mkoa yataendeshwa na uongozi wa mkoa husika ikiwa
ni pamoja na kupanga ratiba yake.
Kwa
upande wa wasichana timu zitakazofungua dimba katika fainali za taifa
ni Ilala na Kinondoni. Kwa ujumla timu 12 zitashiriki fainali za Taifa,
sita za wasichana na sita za wavulana.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Meneja wa Uhusiano wa Airtel
Tanzania, Jackson Mbando alitoa rai kwa makatibu wakuu wa mikoa kuwa
makini wakati wa usajili ili kupata vijana wenye vipaji ambao
wataiwakilisha vema Tanzania kwenye michuanoa ya kimataifa ya Airtel
Rising Stars. Vile vile Tanzania itawakilishwa kwenye klini itakayofanyika chini ya makocha wa Manchester United.
Alisisitiza alisema nia thabiti ya Airtel Tanzania kuendelea kusaidia mashindano ya vijana kwa nia ya kuendeleza soka nchini na kuishukuru TFF na wizara inayohusika na michezo kwa kuyaunga mkono mashindano haya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)