AFISA HABARI AVAMIWA NA MAJAMBAZI, HARUSI YAKE HIVI KARIBUNI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AFISA HABARI AVAMIWA NA MAJAMBAZI, HARUSI YAKE HIVI KARIBUNI


Afisa Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis Nkomola  amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.

Edward Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambao ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.

Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja  mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha, simu na vifaa mbali mbali vya harusi.
 
 Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa  Elizabeth.

Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages