Hili ndilo lori lililopata ajali katika kijiji cha Hanga, iliyotokea jana.
********************************
Watu
nane wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka
kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea kuacha njia na
kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo
mkoa wa Ruvuma .
Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga pamoja na abiria
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki, amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa nne na nusu ( 4:30 ) usiku katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili Mkoa wa Ruvuma, huku ikielezwa kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi, ambapo pia imeelezwa kuwa dereva wa gari hilo alikuwa akiendesha huku akiwa amelewa.
Ajali hiyo imehusisha
gari lenye namba za usajili T.677 ADL aina ya Isuzu lori , mali ya
mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA.
Baada
ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo ametokomea kusikojulikana na
kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya
jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.
Kamanda wa Polisi amesema gari
hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha
vifo vya watu nane(8) na majeruhi kumi na moja (11) ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
Kutokana na
ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki
ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na
abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria.
Pia
ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa
kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka
agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja
ambapo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)