WAREMBO WA "REDD'S MISS TABORA 2013" WAFURAHIA MATEMBEZI KATIKA VIVUTIO MBALIMBALI NA KUJIFUNZA MENGI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAREMBO WA "REDD'S MISS TABORA 2013" WAFURAHIA MATEMBEZI KATIKA VIVUTIO MBALIMBALI NA KUJIFUNZA MENGI

wakifurahi na babu
Warembo wakipozihapa wakiwa na babu atoaye maelekezo katika tembe la makumbusho ya Dr. Livingston
Babu akitoa maelekezo ya historia kwa ufupi huku warembo wakimsikiliza kwa umakini
wakimsikiliza babu kwa umakini mkubwaaa
kweli kuna vitu vingi vya kuvutia
hadi pesa ya zamani
vibuyu hivyo vilivyotumika kuchotea majibabu akiwaonesha matoborwa (viazi vitamu) vilivyozalisha jina la Tabora ikiwa zamani iliitwa Unyanyembe
LIVINGSTONE ALIPOONDOKA TABORA KWIHALA HADI LAKE BANGWERUBEMBA 25/08/1872 (ZAMBIA) ALIPATWA NA MAUTI TAR 1 MAY 1873 (60YRS OLD) ALIZALIWA MWAKA 1813. BAADA YA KIFO CHAKE VITU VYOTE VYA TUMBONI VILITOLEWA NA KUZIKWA KANDO YA ZIWA BANGWERU KIJIJI CHA KITAMBO, MWILI WAKE ULIPAKWA CHUMVI NA KUANIKWA JUANI NA KISHA ULISAFIRISHWA KWA MIEZI 9 HADI BAGAMOYO NA KUHIFADHIWA KATIKA KANISA LA KWANZA LA WAROMA LILILOJENGWA 1868, BAADAYE ZANZIBAR NA KUPELEKWA SCOTLAND ULAYA
kumbukumbuwakila maelekezo ya kutosha toka kwa babu
(ikiwa imebomoka kwa sasa) Ngome ya ulinzi ya mtemi Isike Mwanakiungi aliyotumia kupigania vita na Wajerumani kwa miaka takribani 5 kabla ya kujiua hapo hapo kwenye ngome.
Hapa ndipo ulikuwepo mlango wa ngome (kwa maelezo: ngome hii wakati wa vita hiyo na mjerumani ilikuwa hawawezi kuiona ikiwa nguvu za dawa za kimila ndo zilifanya kazi hiyo)
ilikuwa mbinde kidogo, wamejifunza kuvumilia kutembea katika maeneo magumu
hapa ni katika jiwe ambalo pana maajabu mengi katika historia: Ni eneo ambalo walikuwa wakifanyia uchaguzi wa Watemi, pia maajabu yaliyopo ni kama jiwe kutoa mlio wa ngoma, alama ya kuwekwa mkuki wa mganga wa mtemi Isike Mwanakiungi, pia alama ya alipolala mganga huyo na kucheza bao yeye mganga na walinza pamoja na wanawe.
Mrembo akijaribu kukaa ambapo alama ya makalio ilibaki
sehemu patoapo mlio wa ngoma katika jiwe hilo
warembo wakipiga ngoma na babu (mwelekezaji) akicheza... burudani tupu juu ya jiwe
warembo wakitokelezea kwa picha ya pamoja. PICHA NA: ALOYSON

"WAREMBO WAMEPATA KUJUA MTU WA PEKEE ALIYEZIKWA KABURI MBILI DUNIANI, AMBAYE NI Dr. LIVINGSTON; VIUNGO VYA NDANI VILIZIKWA BARANI AFRIKA NA MWILI WAKE ULIZIKWA BARANI ULAYA"

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages