TIMU YA MWISHO KUTOKA AFRIKA MASHARIKI YASAKA NAFASI YA KUFUZU KUINGIA NUSU FAINALI YA GFC - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TIMU YA MWISHO KUTOKA AFRIKA MASHARIKI YASAKA NAFASI YA KUFUZU KUINGIA NUSU FAINALI YA GFC


  Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tisa(robo fainali ya 4) cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kutoka kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), bluu na kijani ni timu kutoka Cameroon na nyeusi ni yimu kutoka Ghana. 
TIMU YA MWISHO KUTOKA AFRIKA MASHARIKI YASAKA NAFASI YA KUFUZU KUINGIA NUSU FAINALI GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE.

: Jumatano iliyopita kupitia stesheni za ITV na Clouds TV, Waghana Jonathan Naab na Desmond Odaano walifanikiwa kufuzu nusu fainali ya
Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE. Inaweza kusemekana kuwa timu hii ilichagua njia rahisi kwa ajili ya kupata ushindi hadi kufikia hatua ya vikwazo ambapo walikutana uso kwa uso na waghana wenzao.Jonathan na Desmond walifanikiwa kushinda katika vikwazo vyote na kufikia hatua ya ukutawa pesa wa Guinness ambapo walipata  dola za kimarekani 3,000 kuongezea kwenye dola 5,500 walizokuwanazo awali.

Wakiwa na jumla ya dola 8,500 mkononi, Jonathan na Desmond wanajiandaa kutafuta dola 250,000 na ushindi wa Pan-African katika nusu fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.

Watachezea nchi yao pamoja na Emphatus Nyambura na Samuel Papa kutoka Kenya ambao walikuwa washindi wa pili katika robo fainali hyo wiki iliyopita. Katika robo fainali ya mwisho wiki ijayo timu nyingine nne zitaingia uwanjani  kati ya hizo ni timu kutoka Kenya  Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ambao watapeperusha bendera ya Afrika Mashariki ili kupata timu mbili za mwisho.

 “Tumebakiwa na robo fainali moja tu ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE-Je, kuna moja kati ya timu zilizobaki inayoweza kujishindia dau kubwa zaidi ya timu ya Jonathan na Desmond? Washiriki wote wameonesha kuwa wana ujasiri tutaona jinsi timu hizi nne zitakavyocheza wiki ijayo. Ni nani atakayeshinda katika robo fainali ijayo? Tunazitakia timu zote kila la heri katika robo fainali mwisho” alisema Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages