Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya
Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea
kupiga mabomu. Sasa hali si shwari
kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga
mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani
mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila
mwelekeo. Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi
wanakimbia ovyo.
Kituo kimoja cha habari
kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara
hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya
kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)
Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake
kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa
kutoka Mtwara kwenda Dar. Maduka yote yamefungwa, baa
zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya
kimsingi hakuna lolote linalofanyika Boda boda zinazoonekana maeneo ya
Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali. Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.
Credit: Zeddlicious Blog
Credit: Zeddlicious Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)