RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
KUZINDUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA
KM 260 (SEHEMU ZA DODOMA - FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT - MIGORI NA
MIGORI - IRINGA) KWA KIWANGO CHA LAMI TAREHE 22 MEI, 2013
Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, tarehe 22 Mei, 2013 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-
1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2) Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha Migori Wilayani Iringa Vijijini.
Barabara ya Iringa - Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo kama “Great North Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo, Misri kupitia Tanzania. Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma (mpakani na Zambia), Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani na Kenya).
Mradi huu ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara na unalenga kupanua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi, na kati ya Tanzania na nchi jirani za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa njia hii, barabara itakuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Taarifa hii imetolewa na;
Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU
WIZARA YA UJENZI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)