Afisa
Mwajiri wa kampuni ya East Coasts Oils and Fats ambayo ni Kampuni tanzu
ya MeTL Bw. Eric Buberwa akisalimana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete mara baada ya kuwasili katika kampuni hiyo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kusalimiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Lishe.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akiteta jambo na
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakielekea sehemu ya kiwanda cha
East Coasts Oils and Fats. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said
Meck Sadiq.
Afisa
Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya
MeTL Bw. Vijay Raghavan akifafanua jambo kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete kabla ya kukumimina Virutubishi vya Vitamini A katika Kinu cha
kuzalisha mafuta kiwandani hapo ikiwa ni ishara ya kuhamasisha Lishe
bora kwa walaji.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimimina mafuta ya virutubishi katika
kinu cha kutengeneza mafuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kampeni ya
kuhamaisha Lishe bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini
A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani, wakati alipotembelea
Kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS ambacho ni kampuni tanzu ya MeTL
kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Wanaoshihudia tukio hilo ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq (kushoto), Afisa Mkuu
Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL
Bw. Vijay Raghavan ( wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya
MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (wa tatu kushoto) pamoja na wadau wengine
wa masuala ya Lishe.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East
Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL mara baada ya kumaliza zoezi
la kutembelea kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta
ambapo amempongeza Mh. Mohammed Dewji kwa kutengeneza ajira kubwa kwa
Watanzania kupitia kiwanda chake.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya
MeTL wakimsikiliza Mh.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa kwenye
picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya MeTL pamoja na wadau wa masuala
ya lishe alipotembelea Kiwanda cha East Coasts Oils and Fats Kampuni
Tanzu ya MeTL katika Kampeni ya Uongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A
katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Said Meck Sadiq, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh.
Mohammed Dewji (Mb), Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema kwenye picha
ya pamoja na wadau wengine wa masuala ya Lishe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa
Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (kushoto) mara baada ya
kuhutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni
Tanzu ya MeTL. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said
Meck Sadiq na mdau wa masuala ya lishe.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akiagana na Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza ziara yake katika kiwanda
cha EAST COAST OILS & FATS ambacho kampuni tanzu ya MeTL ikiwa ni
mwendelezo wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Lishe bora kwa walaji kwa
kuongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa
viwandani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)