LEO NDIO LEO NANI KUCHEKA AU KULIA NDANI YA UWANJA WA TAIFA...KENDA HAIPO MBALI NA KUMI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

LEO NDIO LEO NANI KUCHEKA AU KULIA NDANI YA UWANJA WA TAIFA...KENDA HAIPO MBALI NA KUMI

 Mashabiki wa Yanga, Kuendelea kurekodi matukio ya furaha Jumamosi??
 Mashabiki wa Simba.....Je Kuendelea na furaha hii Jumamosi???
Mashabiki wa Yanga, Je Simba kupakatwa Jumamosi(LEO)??????
************************************
*Nani kuficha mabango ya utani Jumamosi(lEO)?

Tiketi kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga litakalochezwa keshokutwa (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza kuuzwa kesho (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Vituo vitakavyouza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.

Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages