Okraku Kofi & Isaac Aryee - Ghana
Ephantus Nyambura & Samuel Papa - Kenya
Mei 29, 2013 Jana usiku kupitia televisheni za ITV
na Clouds TV timu pinzani kutoka Afrika zilipambana vikali kufuzu nafasi mbili kuingia
katika fainali ya Pan–African Guinness Football Challenge .
Timu
yetu ya Kenya kutoka Afrika mashariki, Ephatus Nyambura na Samuel Papa
walikusanya alama 14 katika mzunguko wa muundo na wakafikia hadi hatua ya
penati baada ya kuishinda timu ya Cameroon.Wakiwa washindi wa pili wa mchezo
bado wana nafasi ya kushinda katika fainali ya mashindano haya.Waghana Emmanuel
Kofi Okarku na Isaac Aryee walifanikiwa kufikia hatua ya ukuta wa pesa wa
Guinness.
Ephatus,
Samuel pamoja na Emmanuel na Isaac sasa watakutana na Desmond, Jonathan,
Francis Ngigi na Kepha Kimani kufanya timu nne katika fainali ya Pan-African. Hawa
wote wana nafasi ya kupeperusha bendera ya nchi zao, lakini watahitaji
kujiandaa vizuri na kuwa makini ili waweze kushinda taji la Pan-African
Guinness Football Challenge.
Watakaokutana
katika fainali ya mashindano ya Pan-African GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE watakuwa ni timu mbili kutoka Afrika
mashariki na mbili kutoka Afrika magharibi. Kutoka Afrika mashariki ni Ephatus Nyambura, Samuel
Papa, Francis Ngigi na Kepha Kimani.
Ushindani
kati ya Afrika Mashariki na Afrika Magharibi utakuwa mkali,ni upande upi wa
bara utakaoshinda taji hili?
Fainali
ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, yanayoandaliwa na Endemol , itarushwa
na televisheni za ITV na Clouds TV siku ya Jumatano saa 3:15 usiku ITV na saa
2:15 usiku Clouds TV kwa hiyo hakikisha unaangalia mchezo huu huku ukiburudika
na kinywaji cha GUINNESS.
Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa
wale wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)