Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya Jeshi la
Magereza iliyojengwa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa
mbalimbali zilizopo ndani ya Duty Free Shop ya Jeshi la Magereza, Isanga
mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima (kulia). Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja.
Baadhi
ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali baada ya
kuzinduliwa kwa Supermakert (Duty Free Shop) ya Jeshi la Magereza
iliyopo Isanga, mjini Dodoma.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba
fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Pereira Ame Silima kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili
ya kisasa ambayo imejengwa na jeshi hilo, katika Gereza Isanga, mjini
Dodoma. Ufunguzi huo umefanyika leo mjini humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na
maafisa magereza kabla ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili
ya kisasa ya Jeshi la Magereza ambayo itawawezesha maafisa wa jeshi
hilo, askari na familia zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali
kwa bei nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja
na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye
aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Afzal Meghji.
Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa katikati waliokaa),
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja, (wa tatu kushoto waliokaa)
wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa magereza pamoja
na wageni waalikwa baada ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya
kisasa ya jeshi hilo, mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)