Na Onesmo Ngowi, IBF Africa
Tanzania
imetengeneza historia mpya kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada
ya mabondia wake kuwa wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha
nchi na bara la Afrika.
Safari hii
JEMBE, kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas Segu kutoka
katika ukumbi wa mazoezi wa Respect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola
chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma
msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa Thailand pamoja na
nchi za ukanda wa Indo-China.
Segu
alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia Pacific Patomsuk
Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter ambaye ni
bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF.
Mpambano
wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na
kurushwa na television katika nchi zote za ukanda wa Indo-China za Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.
Mpambamo
wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia wa kitanzania kuchomoka kama
upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa makonde
mazito ya kumshikisha adabu. Segu alitupa makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana na uzito na umakini wa ngumi zake Kwa
kipindi chote cha raundi ya kwanza ilimbidi Pathompothong ajilinde na
kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili kudhoofisha masumbwi ya Segu
aliyekuwa anayachanganya kama mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa
kwa wingi nchini Thailand. Jonas Segu
alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George
“Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya
kwenye mpambano huo wa mwaka.
Katika
raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa Thailand kuwa
yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao ila
kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Segu
alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde mfululizo
hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri
kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi
timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya kumdhibiti kijana
huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda Thailand
kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na sio kufuata ulaji! Raudi
ta 5 Pathompothong aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha
msumbwi mfululizo na kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu
kenye kamba ili amkandamizie masumbwi yake. Kijana
huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia na ambaye
wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia ili
kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa
yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya mazoezi ya kutosha.
Segu
alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa
mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye
ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania! Katika
raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na
kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta
kudhibiti harakati za mpinzani mwenza.
Ni katika
kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na
Mthailand Pathompothong. Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia
ili asiendelee kurusha masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia
mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati
Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati wa kitanzania.
Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa hawezi kuutumia mkono wake
vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa anaacha!
Segu
aliacha pambano hilo katika raundi ya saba wakati mashabiki wengi katika
ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania, Tanzania, Tanzania kwa jinsi
alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)