Mmiliki wa JamiiForums na ndugu yake wapata ajali mbaya Nzega - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mmiliki wa JamiiForums na ndugu yake wapata ajali mbaya Nzega

maxence-melo-ajali
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali
maxence-melo-ajali
Habari na picha na AshaDii; at Jamii Forums
Mmoja wa waanzilishi na wamiliki wa Jamii Forums, Maxence Melo, amepata ajali ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza; kilometa chache kutoka Nzega mjini.

Mwanzilishi mwenzie na msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema Maxence na ndugu yake ambaye naye alikuwepo kwenye ajali hiyo, walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
Bw. Mushi amesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana. Haijaelezwa Bw. Maxence melo ameumia kiasi gani, ila taarifa zinasema kuwa ndugu yake amejeruhiwa vibaya .

Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages