Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Salma Kikwete
akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 70 kutoka kwa
Mkurugenzi wa Montage Limited, Teddy Mapunda ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo
katika kuchangia Afya ya Mama na Mtoto. Fedha hizo ni sehemu ya michango ya
wadau mbalimbali iliyopatikana katika harambee maalum iliyopendeshwa na Montage
hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Montage, Zainabu Mkindi (wapili
kushoto)na kulia ni Katibu wa WAMA, Daud Nassib. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
wa ITV, Joyce Mhavile (kushoto0 akizungumza jambo na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda kabla ya kukabidhi hundi kwa
Uongozi wa WAMA.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete (katikati) akisalimina na
Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhavile na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Montage Limited, Teddy Mapunda.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Salma Kikwete (kulia)
akizungumza na Uongozi wa Montage pamoja na wadhamini wa Harambee
iliyoongozwa na Kampuni ya Montage kwaajili ya kuchangisha fedha
kwaajili ya kusaidia matibabu ya Mama na Mtoto nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)