BREAKINNG NEWS:MAHAKAMA YAFUTA KESI YA UGAIDI ILIYOKUWA INAMKABILI LWAKATARE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BREAKINNG NEWS:MAHAKAMA YAFUTA KESI YA UGAIDI ILIYOKUWA INAMKABILI LWAKATARE

LWAKATARE
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere. (33)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages