BREAKING NEWS: BOMU LALIPUKA KATIKA KANISA LA PAROKIA MPYA YA OLASITI JIJINI ARUSHA MUDA HUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BREAKING NEWS: BOMU LALIPUKA KATIKA KANISA LA PAROKIA MPYA YA OLASITI JIJINI ARUSHA MUDA HUU

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE KWENYE MEZA YETU YA HABARI YA LUKAZA BLOG ZINASEMA KUWA BOMU LIMELIPUKA KATIKA KANISA KATOLIKI PAROKIA MPYA YA OLASITI ILIYOKUWA INAZINDULIWA LEO JIJINI ARUSHA MUDA HUU.

BOMU HILO LIMELIPUKA WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO LA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA  NA MPAKA SASA  HAIJAWEZA KUJULIKANA IDADI KAMILI YA WATU WALIOJERUHIWA LAKINI TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU NA MPAKA MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BOMU HILO KULIPUKA.

CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUWA KUNA  GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA BOMU HILO, BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU WENGI WAMEJERUHIWA ZAIDI .

ENDELEA KUWA NASI HAPAHAPA KWA TAARIFA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages