ZIFF waomba filamu za Bongo
UONGOZI
na Wandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi
za Majahazi (Zanzibar International Film Festival (ZIFF) imesema kuwa
imebakisha siku moja pekee kwa wasanii wa Tanzania na wale wa Afrika Mashariki kutuma
kazi zao za filamu zitakazoingia kwenye tuzo mbalimbali za tamasha hilo linalotarajia kufanyika Juni 29 -Julai
7, mwaka huu.
Akizungumza
na .... Mapema leo Meneja wa
Tamasha hilo, Daniel Nyalusi alisema kuwa, toka ZIFF imeitisha upokeaji wa
filamu kwa ajili ya Tamasha hilo la 16 la Nchi za Jahazi mnamo Septemba 2012 na
kuweka mwisho wa kupokea Machi 31, 2013, hata hivyo kukawa na msukumo mdogo wa upokeaji
wa filamu toka Tanzania, tofauti na nje ambapo mpaka sasa wameshapokea filamu
zaidi ya 200 kwaajili ya uchaguzi wa jumla.
“Hii
inasikitisha, mpaka hatua ya mwisho wa
zoezi la kupokea filamu za Kitanzania, ni filamu 5 tu ndio tulizopokea, hivyo kuamua kuongeza muda hadi Aprili 15,
tunaomba wasanii wa Tanzania na wa Afrika Mashariki kuchangamkia siku hizi
mbili zilizobaki ilikutuma kazi zao” alisema Nyalusi.
Pia
Nyalusi alisema kuwa, katika tamasha hilo ambalo mwaka huu linatimiza msimu wa
16, limesheheni mambo mbalimbali na kuwataka wadau kulisubili kwa hamu.
Aidha,
Nyalusi alieleza kuwa, kazi hizo za Swahili Movie/Bongo Movie competition, ndizo filam
zitakazotoa filamu Bora ya Kitanzania, filamu Bora ya Afrika Mashariki na
maeneo mengine (Categories).
Hata
hivyo, Nyalusi alitumia wasaha huo kwa wasanii wote kutuma kazi zao kwenye
tovuti ya ziff ilikutuma kazi zao, ama katika ofisi zao za ndani ya Ngome Kongwe
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)