WEMA SEPETU AFUNGUKA JUU YA KAJALA KUCHEZA MOVIE ZAKE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

WEMA SEPETU AFUNGUKA JUU YA KAJALA KUCHEZA MOVIE ZAKE

Wema Abraham Sepetu
Muigizaji na Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu amesema licha ya kumsainisha Kajala Masanja kwenye kampuni yake, hategemei kumfanyisha kazi kurudisha shilingi milioni 13 alizomtolea kwenye hukumu yake.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL, Wema amesema Kajala atakuwa akifanya kazi zake lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Kwa kuanza Kajala ataigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu iitwayo Princess Sasha.

“Tutaenda kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari fulani hivi kama ya kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess Sasha, she is going to be the main character, “ alisema Wema.

Kwa upande wake Kajala amesema aliamua kujichora tattoo ya jina la Wema kwasababu anamchukulia kama shujaa.“Mi naweza kusema nimeichora kuonesha nimeappreciate vipi kitu alichonifanyia , watu wengine wanaichukulia vibaya, wataongea vibaya, lakini mimi najua moyoni mwangu. Sababu nimeona siwezi kumlipa hiyo hela sasa hivi.

Nitamkumbuka siku zote hata chochote kikitokea atabakia kuwa mtu… yaani she is my hero.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages