Washindi wa kipindi cha Nne cha Guinness
Football Challenge, Enphatus Nyambura(kushoto) na Samuel Papana(kulia)
katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and
Flavia Tumsiime jana baada ya ushindi.
Aprili 10, 2013, Dar es
Salaam;
Katika sehemu ya nne jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV,
mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
yalikuwa na ushindani mkubwa
lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza
kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika
hatua ya Pan- Africa. Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi
kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama
nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya
walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta wa
pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani 1,500.
Enphatus na Samwel wana
nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo
wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita
cha fedha za kimarekani hadi kufikia
dola 250,000. Katika sehemu ya tano ya mashindano
haya, yanayorushwa na vituo vya Televisheni vya ITV na Clouds TV timu nne mpya zitaingia
uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kuendelea na mashindano hata kuingia hatua
ya Pan-African. Je timu nyingine ya Kenya inaweza kushinda?
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila
Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia
saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku
ambapo Clouds TV itarusha kipindi
hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Tafadhali kunywa
kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)