Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Lazaro
Nyalandu akikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza bwana Dicksoni Marwa.
washiriki wakijiandaa tayari kwajili ya
kuanza mashindano wakiwa pamoja na Naibu waziri wa maliasili na utalii
Mh, Lazaro Nyalandu pamoja na waandaaji
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake bi Jacquline Salum toka
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwatoka washiriki wenzie
mwimbaji wa bongoflava Barnaba akiwa na Irene Kiwia manager director kutoka Frontline Porter
Novelli ambaye pia alikuwa mshiriki wa
miss Tanzania wakishiri mbio hizo ambapo walifanikiwa kumaliza mpaka mwisho
Mh, Lazaro Nyalandu akimtoka Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Anthony Mtaka katika mbio hizo
Mh, Lazaro Nyalandu akimtoka Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Anthony Mtaka katika mbio hizo
Dickson Marwa afanikiwa kuichukulia kitita shillingi millioni moja za
kitazanzania baada
ya kuibuka mshindi wa Tigo Ngorongoro
nusu Marathon ambapo mshindi wapili bwana Stephano Huche ambae nae ni aliweza kuondaka na kitita cha
shillingi laki tano.
mashindano haya ambayo lengo lake ni kuhamasisha mapambano
dhidi ya ugonjwa wa malaria yameandaliwa na taasisi tanzu ya kujitolea ya
kampuni ya Utalii ya ZARA Tanzania Adventures ambayo husaidia shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujitolea na kudhaminiwa na kampuni ya Tigo.
akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Maliasili
na utalii Lazaro Nyalandu alisema kila hatua moja ambayo atakuwa anakimbia
mkimbiaji itakuwa inahamasisha umoja katika kupambana na malaria hatua hiyo pia
ni ishara inayoonyesha nia njema ya
waandaaji wa mbio hizo kutokana na lengo la kupambana na ugonjwa huo hatari
unaoua wananchi wengi
"Kwa takwimu tulizonazo hadi sasa ni kwamba malaria
inaua watu zaidi 888,000 barani Afrika na robo tatu wa watu hao ni watoto wenye
umri chini ya miaka mitano na kwa hali hiyo, mbio hizi zinachagiza uhamasishaji
wa kupambana na ugonjwa huo" alisema
Mbio hizo ambazo zinafanyika kila mwaka zimeshirikisha vilabu
26 kutoka Tanzania nzima zilizo na wanariadha 236, zilianzia katika geti la
kuingilia kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizikia katika uwanja
wa Karatu mjini.
Kwa upande wa wanawake, mwanariadha Jacquline Salum toka
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliibuka mshindi na kujinyakulia
kitita cha shilingi laki tano, akifuatiwa na Zakia Mrisho aliyejinyakulia
shilingi laki tatu.
akizugumza Mkurugenzi wa Zara Tours Leila Ansell ambao ni
waaandaaji wa mashindano hayo alisema mashindano ya Mwaka huu wamepata
washiriki wengi zaidi ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kupambana na
ugonjwa na Maralia pia ni kuunganisha pamoja watalii na wananchi wa Tanzania
pamoja na kukusanya fedha zitakazotumika katika mapambano ya ugonjwa hatari wa
Malaria.
aidha mashidano hayo yalianza mapema saa 12:00 asubuhi leo
kwa mbio za watoto kuazia eneo la Mnadani, Karatu, mbio za wakubwa za km 21
zilianzia geti kuu la Ngorongoro na kumalizikia viwanja vya mazingira bora
Karatu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)