Mhandisi wa Kampuni ya Dr Gogo engineering limited, Godwin Kalaghe (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo nyaraka za taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Makanya, wilayani Same juzi. Ujenzi wa kisima hicho uliogharimu sh. mil. 51.6 ulifadhiliwa na TBL.
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo
akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Makanya, wilayani
Same, Asia Zuberi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa kisima cha
maji kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 51.6. Hafla hiyo
ilifanyika kijijini hapo juzi.
Mradi wa
kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania katika
kijiji cha Makanya wilayani Same chenye thamani ya shilingi milioni
51.6.Uwepo wa kisima hiki utasaidia kupunguza tatizo la maji hususani
kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)