Mheshimiwa
Angellah Kairuki(MB),Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiwa namwenyeji
wake Mhe.Sayid Ashraful Islam, Waziri wa Serikali za Mitaa Maendeleo
Vijijini na Ushirika(Wizara inayoshughulika na Usajili wa Vizazi
naVifo)wakati wa ziara yake nchini Bangladesh
kujifunza namna ambavyo nchi hiyo imewezakufikiaa silimia zaidi ya 95 ya
usajili wa
Vizazi naVifo.
Mheshimiwa Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari
wa Bangladesh
Mheshimiwa Angellah
Kairuki akifafanua jambo kwa Mhe.Mhe. Hassanul Haq Inu, Waziri wa
Habari wa Bangladesh wakati wawili hao walipokuwa wakisubiri kukutana na
waandishi wa habari wa Bangladesh na kueleza madhumuni ya ujumbe wa Tanzania
kwenda nchini Bangladesh kujifunza namna ya kuboresha mfumo wa usajili wa vizazi
na vifo hadi kufikia asilimia mia moja (100%).
Mhe. Angellah Kairuki akielezwa jambo na Bw. Nazrul
Islam, Mtendaji Mkuu wa Dhaka South City Corporation
Mhe.
Angellah
Kairuki katika picha ya pamo jana Sir. Fazle Abed, Mwanzilishi na
Mwenyekiti wa taasisi ya BRAC alipotembelea Makao Makuu ya BRAC.
Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe
wake wa wataalam kutoka Taasisiza RITA, NIDA, TRA, Serikali zaMitaa, e-Government,
Tumeya Taifaya Uchaguzina Ofisi ya Takwimu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wenyeji wake.
----
USAJILI
WA VIZAZI NA VIFO NCHINI
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Angellah Kairuki aliongoza ujumbe
wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh tarehe 5-11 Aprili 2013.
Ujumbe huo uliojumuisha wataalam kutoka taasisi mbalimbali za Serikali zinazojihusihana masuala ya usajili ikiwa ni pamoja na RITA, NIDA, TRA, Serikali za Mitaa,
e-Government,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Takwimu ulikwenda kujifunza namna ambavyo nchi ya Bangladesh ilivyoweza kufanikiwa katika zoezi
la Usajili wa Vizazi naVifo kwa zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wao.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri na ujumbe
wake walijionea jinsi ambavyo zaidi ya huduma 16 muhimu nchini Bangladesh
zilivyounganishwa na Mfumo wa kusajili vizazi na vifo na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa.
Huduma hizo ni pamoja naVitambulisho vya Taifa, Leseni ya Biashara, Kitambulisho cha
mlipa Kodi (TIN), leseni ya kuendesh agari, hati ya kusafiria, leseni ya ukandarasi,
vibali vya ujenzi, leseni ya kusafirisha na kuagiza bidhaa ndani na nje ya nchi,
kuunganishi wa huduma muhimu kama umeme, maji, simu n.k. bila kuwa na cheti cha kuzaliwa mwananchi wa
Bangladesh hawezi kupata huduma moja wapo kati ya hizo.
Serikali kwa kutambua umuhimu na faida za kusajili vizazi na vifo,imedhamiria kuboresha mfumo wa Usajili na kunyanyua kiwango
cha Usajili kwa kuanzisha Mpango wa Usajili wa Watoto wote walio na umri chini yaMiaka Mitano
(Under Five Birth Registration Initiative(U5BRI) na mpango wa usajili wa watoto wenye umri wa miaka
6-18.
Katika mpango huu waUsajili,mtoto atasajiliwa na kupatiwa cheti papohapo,
na hivyo kufanya zoezi zima la usajili kuwa la hatua moja badala ya hatua mbili zinazotumika sasa,
yaani kusajili kwanza kisha kupata cheti baadaye. Pia Mpango huu unalengo la
kugatua madaraka ya shughuli za usajili kutoa Serikali Kuu na kupeleka katika Serikali za Mitaa na Vituo vya Afya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)