Shabani Mhamila 'Star Boy' |
Ibrahimu Class 'King Class Mawe akioneshana ujuzi wa kutupiana makonde na Shabani Mhamila 'Star Boy' |
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana
umwamba wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yanayo
endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano
wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA
Sabasaba .Picha na www.superdboxingcoach. |
Na MWANDISHI WETU
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' anaendelea kujifua kwa ajili ya
|
kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali. Pambano la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwala vuta nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema. Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa kumchakaza Jibaba ili kuendelea kujiwekea sifa nzuri. "Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na Mashali" alisema Super D na kuongeza Star Boy
alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa
kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua
kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo
uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta
Boy mwenye rekodi ya .won 14 (KO 5)
+
lost 7 (KO 4)
+
drawn 2
=
23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga Theodor Luanda Frebruary 2,1996 na kutetea vema 10 Februar1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa
Super D Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwakatika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila,Japhet Kaseba,Hassani Matumla,Rashidi Matumla dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis Miyeyusho, Said Mundi na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' pamoja na mabondia mabingwa wa dunia
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)