NANI KUIBUKA MSHINDI JUMATANO HII KATKA MASHINDANO YA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE! - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

NANI KUIBUKA MSHINDI JUMATANO HII KATKA MASHINDANO YA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE!



 Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha nne cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania –bluu, Uganda- kijani na nyeusi.

April 3, 2013, Dar es Salaam; Jumatano iliyopita  kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalionesha ni jinsi gani utulivu unavyosaidia katika mashindano ambapo timu kutoka Kenya ilifanikiwa kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka Kenya . Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na kufikia hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.

Kenneth na Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .

Katika Episodi ya nne ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.

Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha nne wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.


Timu ya blu-Tanzania:
·         Lukwesa Kanakamfunu(18) na Hamza Ziada(20), wote kutoka Dar-es-Salaam wanaojivunia kuwa marafiki japokuwa wanashabikia timu mbili adui yaani Arsenal na Manchester United. Lukwesa ni mwanafunzi na ndiye kichwa cha timu wakati Hamza ndiye atakayekua akionesha uwezo wa kuchezea mpira.

Timu nyekunndu:
·         Ephatus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) wote kutoka Nairobi watashiriki kuona kama wanaweza kuwa timu ya tatu ya Kenya kupata nafasi ya kufuzu mashindano ya Pan Africa. Empantus meneja wa ujenzi na ndiye kichwa cha timu wakati Samuel ambaye ni mchezaji wa Nakuru Allstars FC ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.

Timu ya kijani-Uganda:
·         Andrew Mpanga(30) na Gadafi Mohammed Anguzu(18) wote kutoka Kampala,Andrew ni mshabiki wa Man.Utd wakati Gadafi ni mshabiki wa Man.City.Andrew ni daktari wa meno ambaye atakuwa kichwa cha timu.Gadafi ni mchezaji mpira hivyo ataonesha uchezaji wake.

Timu nyeusi-Uganda:
·         Badi Arorwa(25) na Dennis Bogere(30)kutoka Kampala watawakilisha Uganda katika kipindi kijacho cha mashindano.Badii atajibu maswali akiwa kama kichwa cha timu na Dennis ambaye atakayekuwa akichezea mpira kuonesha kipaji chake.
                               
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.  

Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia  ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.

Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 

*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages