MAANDALIZI YA KUMBUKUMBU YA ALIYEKUWA MSANII NGULI WA FILAMU HAPA NCHINI STEVEN KANUMBA YAENDELEA JIONI HII NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAANDALIZI YA KUMBUKUMBU YA ALIYEKUWA MSANII NGULI WA FILAMU HAPA NCHINI STEVEN KANUMBA YAENDELEA JIONI HII NDANI YA VIWANJA VYA LEADERS

 Msanii wa Filamu Nchini Tanzania Jackline Wolper akiangalia maandalizi yanavyoendelea katika viwanja vya leaders jioni hii kwaajili ya kumbukumbu ya aliyekuwa msanii nguli wa Filamu Nchini Steven Kanumba na mbapo leo itazinduliwa filamu Mpya na ya mwisho kuigizwa na Marehemu Steven Kanumba
 Baadhi ya wafanyakazi kutoka Clouds Media wakiendelea na Uwekaji wa stage kwaajili ya uzinduzi wa filamu mpya na ya mwisho iliyoigizwa na Marehemu Steven Kanumba Enzi za Uhai wake
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na Waigizaji wa maigizo na filamu wanaochipukia wakiwa ndani ya viwanja vya leaders jioni hii kwaajili ya kusubiria uzinduzi wa filamu hiyo na kumbukumbu ya kumuenzi Marehemu Steven Kanumba.
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiwahi viti kwaajili ya kushuhudia filamu ya Mwisho kuchezwa na Marehemu Kanumba inayotarajiwa kuonyeshwa jioni hii ndani ya viwanja Vya Leaders

Baadhi ya Vijana wa Maigizo kutoka Vikundi mbalimbali wakiendelea na zoezi la Upangaji wa Viti tayari kwa zoezi la kumbukumbu ya Marehemu Kanumba Kuanza katika Viwanja Vya Leaders jioni hii.
.....................................................
Ni mwaka mmoja sasa umefika tokea Msanii nguli wa Filamu hapa Tanzania Marehemu Steven Kanumba tokea kupoteza uhai wake kutokana na kuanguka chumbani kwake na kupoteza maisha.

Leo ndio Mwaka mmoja umetimia tokea kufariki kwake na leo ndio wanamuenzi kwa Kuzindua filamu yake ambayo aliigiza kwa mara ya mwisho enzi za uhai wake.

Na tamasha hilo la uzinduzi linafanyika katika viwanja vya leaders jioni hii ambapo maandalizi bado yanaendelea kwaajili ya zoezi hilo kuanza

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages