Meneja
Miradi wa Shirika la Plan International Wilaya ya Ilala Daniel Kalimbya
akiongea katika hafla fupi ya kufunga mkutano wa tathmini ya miradi
inayoendeshwa na Shirika hilo kuhusu Ujasiriliamali katika wilaya ya
Ilala.Mkutano huo ulishirikisha wadau kutoka Asasi zisizo za kiserikali,
Vikundi vya vijana na Maafisa wa Serikali.(Picha na Frank Geofray)
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akiongea katika hafla fupi ya kufunga
mkutano wa tathmini ya miradi inayoendeshwa na Shirika hilo kuhusu
Ujasiriliamali katika wilaya ya Ilala.Mkutano huo ulishirikisha wadau
kutoka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya vijana na Maafisa wa
Serikali.
Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano wa tathmini ya miradi inayoendeshwa na Shirika
la Plan International kuhusu Ujasiriliamali wakimsikiliza mgeni rasmi
katika hafla ya kufunga mafunzo hayo wilayani ya Ilala.Mkutano huo
ulishirikisha wadau kutoka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya
vijana na Maafisa wa Serikali.Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano wa tathmini ya miradi inayoendeshwa na Shirika
la Plan International kuhusu Ujasiriliamali wakimsikiliza mgeni rasmi
katika hafla ya kufunga mafunzo hayo wilayani ya Ilala.Mkutano huo
ulishirikisha wadau kutoka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya
vijana na Maafisa wa Serikali.(Picha na Frank Geofray)
Na Frank Geofray.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Bw.Raymond Mushi amevitaka vikundi vya Vijana, Asasi
zisizo za Kiserikali na watumishi wa umma waliopata mafunzo ya
ujasiriliamali yanayotolewa na Shirika la kimataifa la Plan kuyatumia
vizuri katika kuwaletea maendeleo na kuondokana na umaskini.
Bw.Mushi
aliyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mkutano wa kufanya tathmini ya
miradi ya ujasiriliamali iliyokuwa ikiendeshwa na shirika hilo kwa
makundi mbalimbali katika kata zote za wilaya ya Ilala Jijini Dar Es
Salaam.
Alisema
ujasiriliamali ni njia mojawapo ya kuondokana na umaskini na kujikwamua
kiuchumi hivyo kutolewa kwa mafunzo hayo kutawasaidia wananchi kutambua
fursa zilizopo na kuzitumia vyema.
Aidha
aliwaasa washiriki wa mkutano kuwekeza katika elimu kwa watoto ili
kujenga taifa lenye uelewa na maarifa hapo baadae kwa kuwa watoto
wanapaswa kupewa haki yao ya kupata elimu bora.
“Pamoja
na kwamba mtawekeza katika kufanya biashara lakini lazima mhakikishe na
suala la elimu kwa watoto wenu mnalitilia mkazo ili kuweza kuwajengea
maisha bora hapo badaye”Alisema Bw.Mushi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)