Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Bunengi ya Afrika Kusini Bi. Savannah Maziya
akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NDC (National Development Coorporation)
ambaye pia Mbunge Mstaafu wa Jimbo la KwelaNdugu Chrissant Mzindakaya
walipoonana na uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kujadili
namna Kampuni hiyo kwa kushirikiana na NDC katika uratibu
watakavyosaidia katika kuwekeza kwenye miundombinu ya bandari, reli na
barabara kuunganisha Mkoa wa Rukwa Mikoa pamoja na Nchi jirani kuwezesha
rasilimali zilizopo Mkoani Rukwa zinapata masoko yakiwemo mazao,
madini na utalii. Utalii huo ni pamoja na Kalambo Falls maporomoko ya
maji makubwa barani Afika na Bismark Fort iliyokuwa ngome ya wajerumani
iliyopo hapa Mkoani Rukwa.
Muwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu
Moshi Chang’a akiongoza kikao hicho kilichohudhuriwa na muwekezaji huyo,
wawakilishi wa NDC, Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa
na Halmashauri za Wilaya ya Kalmbo na Sumbawanga. Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta akiwa anazungumza katika kikao hicho.
Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwa
anatoa mchango wake juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani
Rukwa kwa muwekezaji huyo.
Afisa katika dawati la Uwekezaji Ndugu Misasi Marco akimwaga sera kutoka katika dawati lake uwekezaji. Picha Zote Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)