Baada ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari zaidi ya 200 kushindwa kupita eneo hilo na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka Mtwara,Masasi,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Liwale,Nanyumbu na Tunduru kufanya safari kwa kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa huduma kwa Jamii
Kufuatia hali hiyo.
baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa Wakala wa Barabara Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa salama ikiwa pamoja na kutafuta jitihada za haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa yatakayochangiwa na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu
Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.Picha na Mdau Abdulaziz Lindi.
Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.Picha na Mdau Abdulaziz Lindi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)