Richard Commey (kushoto) akimshindilia konde zito mpinzani wake nchini Uingereza
wakati wa ukweli uliokuwa unangojewa kati ya ni nani haswa atayekuwa ubingwa wa
uzito mwepesi (lightweight) katika bara la Afrika kati ya Richard Commey na Bilal
Mohammed wote mabondia kutoka Ghana umewadia na sasa zimebaki siku tatu (3) tu. Mabondia
hao ambao wamekuwa wanajifua kweli kweli kwenye fukwe mbalimbali za jiji la
Accra, watapanda ulingoni siku ya Jumamosi tarehe 8 Machi katika mpambano ambao
unategemewa kuwa waburudani tosha kutokana
na ujuzi wa wote wawili.
Promota wa Richard Commey bwana Michael Amoo-Bediako ambaye anaishi
nchini Uingereza na anayemiliki klabu nyingi za afya (Health Clinics) pamoja na
kumbi za kufanyia mazoezi (Gymnasiums) katika nchi mbalimbali za Ulaya ana matumaini
makubwa sana ya kuinua viwango vya mabondia wa Afrika akitumia mabondia wa
Ghana.
Bediako amekuwa anamfanyia mazoezi makali sana Richard katika jiji la
London nchini Uingereza ili kuinua kiwango chake cha ngumi na akiwa huko
ameweza kuwasambaratisha mabondia wengi wa Ulaya na Asia.
Bwana Bediako ametumia pesa nyingi sana kuhakikisha kuwa Afrika
inaonyesha kiwango kikubwa katika ngumi na amedhamiria kuamdaa mapambano kila
mwezi.
Suali kubwa ambalo limo katika vichwa vya wadau wengi wa ngumi katika nchi
ya Ghana na nchi zote za Afrika ya Magharibi ni Je? Nani kati ya wawili hawa
ataibuka kuwa Mfalme wa uzito mwepesi barani Afrika?
Suali hili lenye thamani ya dola bilioni moja halitangoja kupata jibu
muda mrefu kwani ni siku tatu tu kuanzia sasa litajibiwa nayo tarehe 8 Machi,
2013.
Imetolewa na:
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)