Mwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama na kulia ni mwimbaji Bonny Mwaitege.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama.
Mwenyekiti wa
maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kuwatambulisha baadhi ya waimbaji watakaoshirika
katika tamasha la Pasaka 2013. (Picha na Habari Mseto Blog)
…………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
WAIMBAJI
Upendo Nkone na Boniface Mwaitege wamesema tamasha la mwaka huu
wamejipanga vilivyo kufikisha neno la mungu kwa waamini watakaojitokeza
siku ya tamasha hilo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, Nkone alisema inaonekana ana wapenzi wengi
zaidi katika nyimbo za kumtukuza mungu ndio maana wamemchagua kupitia
ujumbe mfupi wa simu za mkononi, hivyo ana deni la kuwalipa siku hiyo.
“Nimepata
furaha kwa waamini kutambua kazi yangu, ndio maana na mimni najihisi
nna deni, na nawaahidi kuimba wimbo mpya siku hiyo ambao “Nimebaki na
Yesu” ambao unachochea ibada kwa waamini,” alisema Nkone.
Nkone
alisema uimbaji wa nyimbo za injili ni mgumu iwapo utafanya vibaya na
jamii pia itakukataa ambako pia waamini wanatakliwa kuisoma biblia na
kuielewa sambamba na kumuomba mungu kwa dhati ya kweli.
Naye
Mwaitege alisema amefurahi kupata bahati ya kuwa mmoja wa wahudumu wa
neno la mungu siku hiyo kwa sababu tamasha la mwaka jana hakupata
bahati ya kushiriki kwa sababu alikuwa safarini nchini Kenya. “Mwaka
jana nilitamani kuimba pamoja na Rebecca Malope lakini bahati haikuwa
yangu, ingawa nimepata bahati ya kuimba na Sipho Mwakabane ambaye naye
anatokea Afrika Kusini kama Malope na Watanzania wenzangu kama akina
John Lissu, Upendo Kilahiro na Rose Muhando,” alisema Mwaitege.
Aidha
Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex
Msama alisema siku ya Tamasha utafanyika uzinduzi wa albam ya kundi la
Gloria Celebrations ‘Kwetu Pazuri’ itakayojulikana kama ‘Kuweni Macho’
ambayo itauzwa siku hiyo.
Tamasha
hilo ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Mbeya Aprili Mosi, Iringa
Aprili 3, Aprili 6 mkoani Dodoma na Mwanza Aprili 7. Viingilio
katika tamasha hilo kwa VIP ni shilingi 50,000, Viti maalum shilingi
10,000, Viti vya kawaida 5000 na watoto shilingi 2000.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)