PAMBANO LA UBINGWA KUPIGWA April 7 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

PAMBANO LA UBINGWA KUPIGWA April 7

Pambano la ubingwa wa taifa limeandaliwa  kufanyika tarehe saba mwezi wa nne katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwanayamala kwa kuwakutanisha mabondia wanaochipukia kwa kasi nzuri wa uzito wa light fly Shaban Madilu “Tyson” mwenye rekodi ya mapambano 22 kashinda 12(4kwa ko) kapigwa 6 na kadrow 4 atazipiga na Issa Omar “peche boy’ mwenye mapambano 15 kashinda 12(3 kwa ko) na kadrow 3 hajapigwa , kwa hiyo wana sifa za kugombania ubingwa huo wa taifa wa TPBO kwani ubingwa huo kwa sasa hauna mwenyewe  upo wazi kugombaniwa kwa mabondia wenye sifa kama walizonazo Shaban Madilu na issa Omar.

Waandaaji wa pambano hilo Abuu chaka na Bigright Promotion wamelipeleka pambno hilo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma kwa kuwa kuna usalama mzuri na pakingi kubwa ya magari na ukumbi huo umekarabatiwa  ndani na kuwa katika hali nzuri na migahawa ya chakula na vinywaji na baa ya kisasa ipo ndani isitoshe kutakuwepo na mapambano makubwa ya utangulizi wa mabondia wazoefu na wakongwe wa ngumi kama Joseph Marwa atazipiga na Amour mzungu ,wakati ramadhan Kido akipimana ubavu Musa mbabe hawa ni mabondia wa uzito wa juu watazipiga raundi nanenane, pia husein mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atazipiga na Faraj Sayuni, Josef piter”mbowe”(mototo wa golikipa wa zamani wa simba piter paulo) atazipiga na Zumba kukwe  na mapambano mengineyo mengi ya vijana wanaochipukia kwa kasi katika fani ya masumbwi nchini ili kuviimarisha vipaji vyao kwa maandalizi ya kutoa mabingwa wengine wa baadae wa dunia, mapambano haya hayajapata mfadhili wala mdhamini kwa hiyo wanaombwa wajitokeze kuusaidia mchezo huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages