Kaka Lukaza, tafadhali naomba
uniwekee hii post, usinibanie. Siku ya Jumamosi
(23 Machi 2013) nilikuwa na safari ya kutoka Arusha kurudi Dar es Salaam kwa
kutumia usafiri wa ndege wenye ‘jina kubwa’ hapa Tanzania, Precision Air! Kama
unavyofahamu, siku hizi wana-flight za moja kwa moja kutokea Arusha Airport
kwahiyo nilikuwa sina wasi wa kupanda shuttle mpaka KIA ili kuweza kurudi kwa
familia yangu Dar es Salaam.
Mimi na abiria wenzangu tulitakiwa
kuondoka Arusha saa 7 na dakika 20, kumbuka tangia saa 4:45 tulikuwa airport
kwa kukamilisha utaratibu wa check-in time.
Kwenye saa 6 mchana tuliambiwa tukafanyiwe ukaguzi wa mwisho wa usalama
kabla ya kuondoka lakini cha kushangaza baada ya nusu saa kuna mfanyakazi mmoja
wa shirika hilo aliyejitokeza na kwa
bila kutumia lugha ya staha alituamrisha kuwa sasa tumebakia na option mbili;
kupitia Zanzibar au kusafirishwa hadi KIA nakuwahi ndege inayofuata
kuelekea majumbani kwetu Dar es Salaam. BILA
HATA KUTOA SABABU AMA KUTUOMBA RADHI! Abiria tuliwaka kweli kweli! Hapo
tumeshachoka, tunanjaa, na hako kajamaa hata hakataki kutusikiliza!
Anyways, Precision Air waliweza
kuruhusu abiria kama 10 kupitia Zanzibar – Nairobi – Dar es Salaam (ambayo hata
hivyo sijui kama walifika saa ngapi), huku sisi masalia wengine kama 25 hivi tukapandishwa
kwenye mkweche wa basi kuelekea KIA (picha nimeambatanisha hapo kwenye email). Hapo
hapo sisi tuliopandishwa kwenye hiyo basi iliyochoka na kutoa harufu kweli
kweli hatukuambiwa hata hiyo ndege tutakayoenda kuipanda KIA inafika na
kuondoka saa ngapi. Ni cha kushangaza sana kwamba mfanyakazi wa Precision Air
aliyetuamrisha kwenda KIA alikuwa hana majibu haya!
Ndugu zangu, tumefika KIA bado
tukakuta bonge la foleeeeni linatusubiria mpaka kufika ticketing counter! Huku
tukiambulia machungu ya safari maana mpaka sasa hakuna mtu aliyetuomba radhi
(kumbe makubwa zaidi yalikuwa mbioni kujitokeza)! Tumefika counter kwa nguvu
zote ndo tunapewa taarifa kwamba ndege inayofuata inaondoka saa 2 na dakika 20
USIKU! Ambayo nayo ilipata delay mpaka saa 4 zaa USIKU! YAANI NIKAJIKUTA
NIMEFIKA NYUMBANI SAA 6 ZA USIKU! UCHOVU, NJAA NA BADO SIJAOMBWA RADHI!!!
Maskini pia kuna wazungu wa watu
ambao walikuwa wana International flight hiyo saa 4 usiku nao wakaponzwa na huu
uzembe wa Precision Air!!! Embu angalia jinsi ilivyoweza kutzalilisha kitaifa
pia!
Jamani wadau, Precision Air sio
ndege yakupanda!!! Kama mnasafari zenu ni bora mkachungulie ndege
zingine..bahati mbaya ushindani kwetu si sana ndo maana hata hii shirika la
ndege inajitia kiburi kiasi hiki!!!
Kwangu mi binafsi sitapanda tena
ndege ya Precision Air!! Nikikosa ndege ingine ni bora nikapande
basi..ntajipangilia mi muda wangu binafsi wa kufika.
Kama Precision Air hawataweza
kujirekebisha ni bora wakaifunga hiyo biashara, maana ni dhahiri kwamba
hawaiwezi!
Napenda kuwasilisha.
Mdau.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)