Maisha ya polisi: Wengi wanaishi chumba kimoja - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Maisha ya polisi: Wengi wanaishi chumba kimoja

Baadhi ya askari polisi wakisukuma gari lao lililoharibika katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam Machi mwaka huu . Picha na Maktaba. 
---
 Baadhi ya askari polisi wa chini wanaishi maisha magumu kutokana na kupata kipato kidogo huku wakiishi katika nyumba duni hali inayofanya utendaji wao kushukaBaada ya shughuli nyingi za kutwa nzima, askari polisi Hashim (siyo jina lake halisi),  anarejea nyumbani kujipumzisha.

Kwa kuwa nyumba anayoishi ipo umbali wa mita 700 kutoka katika  kituo chake cha kazi, Hashim anaamua kutembea kwa miguu.

Anafika nyumbani huku akitokwa jasho mwilini, lakini kabla ya kuingia ndani anawaza mengi, ikiwa ni pamoja na joto lililopo katika nyumba anayoishi na mke wake pamoja na watoto wao wawili.
Nyumba hiyo ni ya chumba kimoja na pia imeezekwa kwa mabati kuanzia juu mpaka chini.

Licha ya kukaribishwa kwa furaha na mkewe, Hashim anaingia ndani kwa unyonge, baada ya kubadili nguo za kazi anakwenda kuoga katika bafu la nje, ambalo hutumiwa na familia zaidi ya 20 za polisi wanaoishi katika nyumba za jeshi hilo (Kota) takriban 25 zilizopo Mtaa wa Mizengo (siyo jina halisi).Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.....>>>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages