FOR IMMEDIATE RELEASE – Friday, March 1st,
2013 -Dar-Es-Salaam,
TANZANIA- Mabondia Richard Commey na Bilal
Mohammed wote wa Ghana kesho watapima uzito kwenye viunga vya Lebanon katikati
ya jiji la Accra, nchini Ghana kwa mpambano wao wa kutafuta Mfalwe wa uzito mwepesi
katika bara la Afrika. Maandalizi haya ni pamoja na kuwaleta maofisa watakaosimamia
mpambano huu ambao wote wameshawasili katika jiji la Accra wakiongozwa na Rais
wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Masharikiu ya Kati, Mtanzania
Onesmo Ngowi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola
(CBC).
Maofisa wengine watakaomsaidia
Ngowi ni pamona ja refarii Rodger Barnor kutoka Ghana na majaji Fred Ghartey, Confidence Hiagbe na May Mensah
Akakpo wote wanatoka katika nchi ya Ghana.
Zoezi la kupima uzito na afya za
mabondia hawa litaanza rasmi saa nne asubuhi katika Hotel ya Coconut Groove
Regency iliyoko karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kutoka jijini Accra.
Mpambano huu unafanyika baada ya
pambano kubwa lililokuwa liwakutanishe mabondia Joseph Agbeko wa Ghana na Luis
Mendelez wa Columbia nchi iliyoko Amerika ya Kusini kuhamishiwa tarehe 22
March.
Katika mpambano huu mkubwa,
kulikuwa na mpambano mwingine kati ya Frederick Lawson na Isaac Sowah katika
uzito wa Welter lakini sasa utafanyika
tarehe 22 March pamoja na pambano hili kubwa.
Bondia Richard Commey ni bondia
anayewika kwa sasa na kupanda chati anamenejiwa na Michael Amoo-Bediako
mfanyiabishara maarufu wa Ghana anayeishi katika jiji la London nchini Uingereza
na kufanyiwa mazoezo na Carl Lokko wa Ghana.
Naye Bilal Mohammed bondia wa
siku nyingi na mwenye madaha ulingoni anamenejiwa na kufanyiwa mazoezi na
Yebohey .
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION
AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)