Timu nzima ya Lukaza Blog inapenda
kuwatakia wadau wake na wananchi wote kwa ujumla heri ya pasaka. Mungu
atulinde na kutupigania kila siku katika maisha yetu na tuzidi kuwa
watiifu mbele yake na isiwe wakati wa pasaka tu.
Vilevile Lukaza Blog inajumuika na
Wananchi wote kwa Pamoja katika Kuomboleza Msiba wa
Ndugu zetu, Kaka zetu na wote waliopoteza maisha katika ajali ya kuporomokewa na jengo la ghorofa 15 jijini Dar Mungu atupe nguvu katika Kipindi hiki Kigumu ambacho ni vigumu kwa kila
mmoja wetu kuamini lakini Ndugu watanzania wenzetu tunaomba Tuwe
watulivu na tusihukumu kwa kile kilichotokea ila tusubiri ripoti husika
na Vyombo husika kufanya kazi yao.
Mungu atujalie nguvu,upendo, na
utulivu hasa katika kipindi hiki kigumu.Mungu atuzidishe pale tunapotoa
na kututia moyo haswa katika kazi zetu za halali tunazofanya.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia
tena Heri ya Sikukuu ya Pasaka Na tuwe makini hasa na watoto wetu kwa
kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka
Imetolewa na
Josephat Lukaza
Lukaza Blog Team






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)