Mkuu
wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiwa anakata utepe wa lango la
kuingia katika ukumbi wa World Garden uliozinduliwa leo jijini Arusha.
Ukumbi wa World Garden unavyoonekana kwa mbele.
Ukumbi wa World Garden unavyoonekana kwa mbele.
Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na wageni waalikwa wakitembelea ukumbi wa disco wa World Garden mara baada ya kuuzindua.
………………………………………………………………………..
Na Woinde Shizza ,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa
Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuanza kuwekeza katika
sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa huo katika madhari na hadhi ya
jiji
Aliyasema hayo jana wakati
akifungua jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo
jijini hapa lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata
ya mshono ndani ya jiji la Arusha
Alisema kuwa mkoa wa Arusha kwa
sasa umepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo ni wajibu wa wazawa kuwekeza
katika mambo mbalimbali akitolea mfano kuwa mpaka sasa pamoja ya kuwa
wananchi ni wengi na wageni ni wengi lakini mpaka sasa kuna sehemu
super makerti moja tu kitu ambacho kinatia aibu kwa jiji kubwa kama hili
Alisema kuwa viwanja vipo vya
kujengea sehemu hizo ni watu wa kuwekeza tu hivyo aliwasihi wawekezaji
wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika vitu mbalimbali ili kuweza
kuwezesha jiji letu kuwa la kimataifa
Alibainisha kuwa wafanyabiashara
wakubwa wamekuwa wanaogopa kwenda kuchukumikopo na kuwekeza katika vitu
mbalimbali lakini aliwatoa hofu na kuwaambia kuwa mikopo ipo na ni haki
ya kila mmoja kwenda kuchukuwa mkopo kwani nafasi zipo wazi na mikopo
ipo ya kutosha huku akibainisha kuwa amna mfanyabishara yeyote mkubwa
anafanya kitu pasipo kuchukuwa mkopo
Alipongeza uongozi wa kampuni ya
World Garden na kudai kuwa wameweza kupiga atua kubwa kwani kufungua
kwao kwa jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kwani vijana wengi
watapata ajira kupitia jengo hilo kwani katika jengo hilo kuna vitu
vingi kwama vile ukumbi wa disco watu wa usafi wa nje na mengine mengi
ambapo watu wote wanaotakiw akufanya kazi huku ni watanzania vijana
hivyo watakuwa wamesaidia vijana kupata ajira
Kwa upande wake mkurugenzi
mtendaji wa World Garden alisema kuwa wao kama kampuni yao inampango wa
kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 120 na pia alisema kuwa watajitaidi
kuboresha vitu mbalimbali .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)