Watalii wafurika Serengeti kushuhudia tukio la Nyumbu kuzaliana - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Watalii wafurika Serengeti kushuhudia tukio la Nyumbu kuzaliana

Kundi la Nyumbu madume wakiwa wamejikusanya pamoja Serengeti wakiangalia watoto wao wanavyofurahia mandhari ya SerengetiKundi la Nyumbu madume wakiwa wamejikusanya pamoja Serengeti wakiangalia watoto wao wanavyofurahia mandhari ya Serengeti
Ndama hawa wakirukaruka katika mandhari nzuri ya SerengetiNdama huyu wa nyumbu hachezi mbali na mama yake kwa ajili ya kunyonya.Picha Kwa Hisani Ya Fullshangwe Blog
………………………………………………………………
Zaidi ya Watalii 16,500 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni miongoni mwao wakiwemo Watanzania 5,800 wamefurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia tukio adimu linalohusisha Nyumbu wapatao elfu nane (8,000) kuzaliwa kila siku.

 Mwezi Februari kila mwaka ndipo msafara wa Nyumbu hufika katika eneo la kusini mwa Serengeti kwa ajili ya kuzaliana. Miongoni mwa wageni waliofika Serengeti mwaka huu kushuhudia tukio hili muhimu ni pamoja na watafiti wa wanyamapori na wanazoolojia wanasayansi maarufu sana ulimwenguni.

 Msimu wa Kuzaliana katika Serengeti ni tukio la kipekee ambapo ni Serengeti pekee duniani ambapo wanyama hawa huzaliana kwa pamoja katika mzunguko wao wa mwaka mzima.

 Msimu huu wa kuzaliana utadumu kwa muda wiki sita ambapo hadi kukamilika kwake inatarajiwa kuwa ndama wapatao 500,000 watakuwa wamezaliwa katika eneo la Serengeti ambayo ni hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania.Kinchosisimua zaidi katika tukio hili ni pale ambapo nyumbu hawahitaji kulala chini kwa ajili ya kuzaa bali tukio hili huendelea huku Nyumbu akiwa anaendelea kutembea na kula malisho ya majani hifadhini.

 Cha kipekee zaidi ni pale ndama aliyezaliwa mara tu akishazaliwa, humchukua kati ya dakika mbili hadi tatu kuanza kurukaruka na kumfuata mama yake kwa kasi kubwa.

 Hata hivyo miongoni mwa ndama hawa wanaozaliwa kipindi hiki, wengi wao wapo hatarini kuliwa na wanyama wakali wanaowawinda kwa hamu kubwa kwa ajili ya kujipatia chakula. Wanyama hawa maarufu kwa kuwinda ndama hawa ni pamoja na fisi wanaofikia 7,500 pamoja na simba zaidi ya 3,000 ambao wote hukodolea macho tukio hili kwa nia ya kujipatia mlo wao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages