Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika
linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky Mketema
kulia na wajumbe wenzake wa shirika hilo watatu waliosimama nyuma. Kulia
waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Frank Mateni na kushoto aliyekaa ni
Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Deonisya Njuyui.
Mama Maria Chambanenge mlemavu wa
ngozi anayenyonyesha mtoto wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa ambao
wameshatiwa nguvuni na jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake uliokatwa
umeshapatikana. Upelelezi bado unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi wanaohusika
na vitendo hivyo.
Mkurugenzi wa shirika la under the
same sun Vicky Mketema ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa
kushughulikia tatizo hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata kiungo
hicho na watuhumiwa waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo mikoa
yote ingekuwa inashughulikia matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo basi
uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili yo.
Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri.Picha Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)