Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akimlaki Mkurugenzi
Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s aliyewasili nchini usiku wa kuamkia
leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. Waliobaki nyuma ni Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou, Balozi wa
Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj na Msaidizi wa Mkurugenzi wa
UNESCO.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) akimwongoza
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s sehemu ya mapumziko kwa
viongozi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal) usiku wa kuamkia leo . Bi. Irina Bokova’s atakuwa nchini kwa ziara ya Kikazi ya siku mbili itakayoanza leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s akisalimiana na Katibu Mkuu wa Natcom
Prof. Elizabeth Kiondo. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa
UNESCO Africa Bi. Lalla Aicha Ben Barka (wa pili kushoto) na Mwakilishi
wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (kulia).
Mkurugenzi
Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s ( wa pili kulia) akizungumza jambo na
mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru
Kawambwa. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Begum Taj
na kulia ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke
Jensen.
Mkurugenzi Mkuu wa
UNESCO Bi. Irina Bokova’s akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawamba kwenye chumba cha mapumziko katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal)
usiku wa kuamkia leo jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wenyeji wake Waziri wa Elimu na Maufnzo ya
Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini
Ufaransa Mhe. Begum Taj.
Dk. Shukuru Kawambwa akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s.
Mkurugenzi
Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s akiondoka katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal) mara baada ya kuwasili
nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)