Mama
Salma Kikwete (MNEC) Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA)
akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa mara baada
ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo. Anaemuongoza ni
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Atakuwepo Mkoani Rukwa kwa ziara ya siku tatu ambapo atakabidhi msaada
wa vifaa vya hospitali kutoka WAMA, atafanya mkutano na wanawake,
atakabidhi pikipiki za mradi wa PMTCT katika tarafa ya Matai Wilaya mpya
ya Kalambo, atakabidhi pia vitambulisho vya matibabu ya wazee wa
Manispaa ya Sumbawanga, na vilelvile kabla ya kuondoka atafanya mkutano
na wanajumuiya wa shule ya St. Theresia ya Mjini Sumbawanga.
Mama Salma akiveshwa Skafu na moja ya Skauti mara baada ya kuwasili Mkoani rukwa.
Mama Salma akifurahi na vikundi vya ngoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mama
Salma akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mkoa wa
Rukwa Aeshi Hillal ambae pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini
CCM. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Ignas Malocha.
Mama
Salma Kikwete akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga Mkoani Rukwa leo mara baada ya
kuwasili katika ikulu hiyo kwa ajili ya mapumziko mafupi, chakula na
kusomewa taarifa ya Mkoa.
Mama
Salma Kikwete Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitaka
ufafanuzi wa jambo kutoka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
wakati akimsomea taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika sekta ya afya.
Kutoka
kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, wa
tatu ni Ndugu Aeshi Hillal Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa
Rukwa, Iddi Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na Mussa Chang’a Mkuu wa
Wilaya ya Kalmbo wakifuatilia taarifa hiyo iliyokuwa ikiosmwa na Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa.
Mganga
Mkuu Hospitali Kuu ya Mkoa Rukwa Dkt. Gurisha Richard akifafanua jambo
kwa Mama Salma Kikwete juu ya vifo vya mama na mtoto Mkoani Rukwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Mama Salma Kikwete
taarifa hiyo ya Mkoa wa Rukwa kuhusu sekta ya Afya. Katika taarifa hiyo
Mama Salma kikwete aliutaka uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kutoa
elimu kwa kina mama kabla na baada ya kujifungua ili kupunguza vifo vya
mama na mtoto ambavyo vingi husababishwa na uelewa mdogo wa akinamama
juu ya afya zao na watoto.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)