KATIKA PITAPITA ZANGU KWENYE FACEBOOK NIKAKUTANA NA HUU UJUMBE, UJUMBE HUU NI MARA YA PILI SASA NAKUTANA NAO AMBAPO MARA YA KWANZA NILIKUTANA NAO MWAKA JUZI NA MWAKA HUU UMEJIRUDIA TENA NIKAONA SIO MBAYA KAMA NA WENGINE WAKAKUTANA NAO...
Mi ni graduates wa chuo kimoja cha uma mwaka 2010 and nakummbuka sana
stories tulizokuwa tunapiga enzi za chuo na matumaini kibao na washkaji
chuoni, especially ambao tuliingia chuo direct from school ambazo mara
nyingi zilikuwa tofauti na stories ambazo in services walizokuwa
wanaziongelea wakitokea makazini,, so after almost a year In real
practical world nimejifunza yafutayo na nimeona si vibaya nikishare na
washkaji zangu ambao bado mkpo vyuoni na mtaani mkiendelea na harakati
1.Kwanza kabisa Heshima kwa watu wote ama course yoyote sababu vyuoni
kuna tabia ya kujiona huko juu kisa unasoma course flani like Telecom,B
com, BAF, logistics etc na kuwaponda wenzako kuwa watasota kitaa au
watakuwa na maisha duni kisa wanasoma degree hazieleweki, in real world
maisha hayaeleweki na ajira siku hizi si mchezo na hata kubebwa lazima
ubebwe na mtu mwenye nguvu kweli kweli sio rahisi kama tunavyozani na
hii imechangiwa na technology, siku hizi kazi nyingi zinafanywa under
management system so haziitaji nguvu nyingi ya lazima kumwajiri
aliyosomea yoyote anafundishwa system kasha anapiga mzigo kama kawa,
2.Pia kuandaa plan B mapema, nadhani wengi wetu plan A inakuwa kuajiriwa
nah ii inaweza ikabuma so ni vyema kuandaa plan B na hata Plan C if
possible mapema na tena itapendeza ukianza nayo toka huko chuoni wakati
unapata pata vipesa vya Boom kama mtaji mdogo wa what ur going to do
kama usipopata ajira.
3. Kuwa makini kwenye Mahusiano yako,
Date the right one sababu patner ndo mtu wa kwanza close kwenye harakati
za maisha na hata kupeana furaha hata kama mishe haziendi sawasawa, na
vyuoni ni sehemu zenye wide choice so badala ya kupoteza muda na
visister duu visivyojua maisha ni nini au visharobaro visivyojielewa
kama ni mdada jilengeshe kwa right man ambae mtakuwa pamoja kwenye
michakato yote coz hukisubiri uje umpate wakati una kazi nzuri au pesa
nyingi atakuwa feki huyo na pia kupata hiyo kazi nzuri na pesa nyingi
inaweza isifike hata baada ya 10 years as soko ni gumu sana nowdays and
Kila nyumba ina graduates siku hizi so job is a real challenge
4.Jitahidi uwe unique katika competitive market usipende vitu vya
kuigana as kufata mkumbo like kukimbilia masters wakati hauna experience
tena kwenye vyuo vyetu vya kibongo ulivyosoma undergraduate unaenda
kuchukua masters cheti, but u ddnt masters anything because the mean of
master is the same as mastering something you know better and wish to
continue doing on your life. But ukipata chance abroad atleast utachange
pia hata kuimprove communication skills as you know kidhungu ni ishu
kwa sisi wabongo. USHAURI HIYO SCHOOL FEES YA MASTER BILA EXPERIENCE NI
BORA HUITUMIE KAMA MTAJI KWENYE PLAN B YAKO kuliko kuipeleka chuoni then
ukarudi kwenye u jobless
5. Communication skills kwa
kiingereza nazo zinahusika nowdays, kwa wale mliopitia English medium
schools au kusoma abroad na wote ambao kiingereza mnakijua vizuri
tumieni lugha hiyo vizuri kuwachanganya mabosi kwenye interviews au hata
kwenye career fairs as you know kwa bongo English deal, although haina
maana yoyote.
6. Pia jitahidi ujichanganye na watu mbalimbali
ili utengeneze network na pia fuatilia sana kampuni ambazo zinarecruit
kila mwaka like KPMG, PWC, DELLOITE, SDV, PKF, ERNST AND YOUNG etc
sababu hizo ndizo hope kubwa kwa graduates tusio na connection sababu
ziko na fair recruitment japokuwa ni process kupata maana interview sio
chini ya tatu na GPA lazima iwe inasoma na ina relate na matokeo ya Form
4 and form 6, sio form4 div 4, form 6 div 3 halafu chuo una first class
hapo jamaa watajua chuo umefanya uchakachuaji tu, Nimesema hivyo
through my experience working in among those firm since I graduate up to
now, na nilipata job bila kumjua hata mfagiaji wa ofisi,, so I
encourage my fellows mjaribu bahati zenu..
NI HAYO TU NDUGU ZANGU NIMEONA TUSHARE KAMA KUNA MTU ANA LA KUONGEZEA RUHUSA KWA FAIDA YA NDUGU NA JAMAA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)