BENKI YA EXIM YAIPIGA JEKI KLABU YA GYMKHANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI YA EXIM YAIPIGA JEKI KLABU YA GYMKHANA

Kapteni wa mchezo wa squash wa klabu ya Gymkhana Akil Hirji (katikati) akikabidhi zawadi kwa Mkrugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (wapili kushoto) kama ishara ya kutambua jitihada za kukarabati viwanja viwili vya mchezo wa squash mwishoni mwa wiki.
                                                   
Mkrugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (katikati) na Mwenyekiti Msaidizi wa Klabu ya Gymkhana William Chiume (wapili kulia) wakikata utepe ulikuzindua viwanja viwili vya mchezo wa Squash vilivyokarabatiwa na benki ya Exim. 


DAR ES SALAAM, Tanzania

KATIKA jitihada zake za kusaidia maendeleo ya michezo nchini, Benki ya Exim Tanzania, imeipiga jeki Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam kwa kuikarabatia viwanja vyake viwili vya mchezo wa Skwashi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya ufunguzi wa viwanja hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant alisema mchango wa benki yake unatokana na kutambua umuhimu wa michezo katika maisha ya kila siku na kwamba anaamini utasaidia kuendeleza mchezo huo. 
 
“Benki ya Exim tumeamua kushirikiana na Klabu ya Gymkhana kukarabati viwanja viwili vya skwashi ili kujenga mazingira mazuri ya uchezaji wa mchezo huo kwa wachezaji. Tunapongeza dhamira ya kitaifa ya Gymkhana, hasa jitihada zake za kujenga uelewa kwa vijana katika michezo,” alisema Grant.

Grant alibainisha kuwa uwekezaji katika michezo ni suala muhimu kama nchi inahitaji kupata mabalozi wazuri wa kuliwakilisha taifa nje ya mipaka na ndiyo maana benki yake imeamua kusaidia ukarabati wa viwanja hivyo, huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano wa Exim katika uwekezaji.

Kwa upande wake, nahodha wa mchezo wa skwashi wa Klabu ya Gymkhana, Akil Hirji, alisema kuwa ukarabati wa viwanja hivyo ni msaada mkubwa utakaoinua maendeleo ya mchezo huo na kusema kuwa klabu itatumia vizuri miundombinu hiyo iliyoboreshwa.

“Naishukuru Exim kwa msaada wao na nina imani utakuza maendeleo ya skwashi nchini. Kwa viwanja hivi vya kisasa, wachezaji watakuwa katika nafasi nzuri ya kushindana kitaifa na kimataifa,” alisema Hirji na kuongeza Gymkhana imeandaa mashindano ya uzinduzi wa viwanja hivyo yatakayohusisha wachezaji 30.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages